Kiungo wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie de Jong ameendelea kusisitiza kua mipango yake ni kubaki ndani ya klabu ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi.
Kiungo Frenkie de Jong amesema anatarajia kubaki ndani ya klabu ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi na anataka kusalia klabuni hapo na kucheza katika dimba lipya la Camp nou, Klabu ya Barcelona ipo kwenye mpango kufanya marekebisho katika uwanja wake wasasa.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo msimu huu, Huku akiwa moja ya wachezaji wa kutumainiwa na muhimu kwa klabu hiyo chini ya kocha Xavi Hernandez na hiyo imekuja baada ya kuimarika kwa kiungo huyo zaidi msimu huu.
Frenkie de Jong ni kama ameikata maini klabu ya Manchester United ambayo imekua ikimfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo, Kwani kiungo huyo amesema haoni akiondoka ndani ya klabu ya Barcelona kwani klabuu hiyo ni klabu ya ndoto yake zake na anafurahi kuwepo hapo.
Klabu ya Manchester United inaelezwa licha ya kauli za Frenkie de Jong lakini bado imepanga kumhitaji tena kwenye dirisha kubw ala usajili majira ya joto mwezi wa sita na wameandaa ofa kubwa kwa klabu hiyo, Hivo kinachosubiriwa ni kama klabu ya Barcelona kama itavutiwa na ofa ambayo imeekwa na Man United.

