Messi Apewa Heshima Tena Kwao

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amepata heshima nyingine tena nchini kwao baada ya chama cha soka nchini humo kurasimisha kituo cha mazoezi nchini humo kuitwa jina la staa huyo.

Kauli ya nabii hakubaliki kwao huo msemo hauna nguvu kwa Messi kwani heshima inazidi kumiminika nchini Argentina kwa staa huyo ambaye amekua akiipambania nchi hiyo kwa muda mrefu sana mpaka kufikia hatua ya kumpa heshima hiyo.MessiRais wa shirikisho la soka nchini Argentina ameamua kuupa uwanja huo jina la gwiji huyo ambaye amerufdisha heshima ya nchi hiyo ambayo ilipotea kwa miaka mingi, Gwiji huyo alifanikiwa kushinda kombe la dunia ambalo taifa limekua likisubiri tangu mwaka 1986.

Messi kwa kushirikiana na wenzake walihakikisha wanarudisha heshima ya taifa lao kwenye medani ya soka kwani ndani ya miaka miwili wamefanikiwa kubeba mataji mawili makubwa, Kombe la dunia ambalo wametwaa mwaka 2022 na kombe la Copa America ambalo wametwaa mwaka 2021.MessiNahodha Lionel Messi amepata heshima hiyo kutokana na mchango wako kwenye timu hiyo kwani mpaka sasa anasalia kama mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo, Huku akiwa kama mchezaji alieshinda kila taji kwenye taifa hilo na kufanikiwa kuvunja rekodi mbalimbali katika nchi hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.