Telles Kurejea United

Beki wa kimataifa wa Brazil anayekipiga klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester United Alex Telles inaelezwa atarejea ndani ya Man United mwishoni mwa msimu huu.

Alex Telles ametolewa kwa mkopo wa msimu mzima na klabu yake ya Man United kwa klabu ya Sevilla ya nchini Hispania, Lakini inaelezwa atarejea mwishoni mwa msimu baada ya mkopo wake kumalizika ndani ya Sevilla kwani hakuna kipengele cha kumnunua jumla.tellesBeki huyo aterejea ndani ya viunga vya Old Trafford mwishoni mwa msimu ili kujadili hatma yake na miamba hiyo ya soka nchini Uingereza, Kwani klabu hiyo haikueka kipingelea kinachowaruhusu Sevilla kumnunua jumla mchezaji huyo endapo atafanya vizuri ndani ya klabu yao.

Beki Alex Telles amefanikiwa kuonesha kiwango bora ndani ya klabu ya Sevilla mpaka sasa na amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya timu hiyo, Kitu ambacho kimewavutia klabu ya Sevilla kutaka kumbakiza beki huyo kuendelea kusalia kwenye viunga vya Ramon Sanchez Pizjuan.tellesKlabu ya Sevilla italazimika kurudi kufanya mazungumzo na klabu ya Man United ili kuweza kumpata Alex Telles kwani beki huyo anasalia kua mali ya mashetani hao wekundu kutoka jijini Manchester, Hivo wanapaswa kukaa mezani na kufanya makubaliano na Man United ili kuweza kumbakiza beki huyo Sevilla.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.