Pengine ni wengi walijiuliza kwanini Alex Telles hakuepo kwenye kikosi cha Man United dhidi ya RB Leipzig. Taarifa rasmi zimeripoti maambukizi ya COVID19.
Alex Telles alijiunga na Man United dirisha la usajili la majira ya kiangazi na ameitumikia United katika mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa (dhidi ya PSG).
Alex hakuwepo kwenye kikosi kilichocheza na RB Leipzig na taarifa rasmi ilitolewa na kocha Ole Gunnar Solskjaer.
“Telles amepata maambukizi ya COVID19 na atakuwa nje ya uwanja kwa muda. Hakuwa na dalili zozote, hivyo yupo sawa na atarejea muda si mrefu.” alisema Solskjaer akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Man United wanaongoza kundi H wakiwa na pointi 6 lakini wapo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa EPL. Jumapili hii watawakaribisha Arsenal katika dimba la Old Trafford.
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.



aisha
Corona imekua tishio kwa wachezaji wengi pole sana telles kwa kuugua
Sabrina
Duuh pole yake
Elika
Dah pole sana..Mungu yupo hakika atapona
Fatina mfigi
Pole mungu hatakufanyia wepec utapona
Dorophina
Corona inaendelea kuwa tishio
warda
Huu Ugojwa jamani Sio Poa
Ernest
Mkosi mwingine kwa Man U huu
Khadija
Ugonjwa huo sasa ushakuwa tishio kwa wachezaji
zeiyana
korona hatari sana
Adelta
Hili gojwa sio poa kabisa mwenyezi mungu atuepushiye
Sauda
Pole yake
Lydia Emmanuel Magoti
Daa pole yake
Carolyn
Aendelee kuchukua tahadhari ili asiambukize wengineee
Mwajumah
Corona sio poa kabisa
Hopemwaikuka
Pole sana
Issa
Inabid timu ipate uangaliz zaid ili kupunguza kuenea zaid
Povel
Get well soon
Saupha mohamed
Duuh corona nomaa sana
Fatuma kasomo
Poa yake