Southgate Achukizwa na Rashford

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza  Gareth Southgate ameonesha kuchukizwa na kitendo cha mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford baada ya kujiondoa kwenye timu hiyo.

Kauli ya kocha Gareth Southgate baada ya kupata ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Italia siku ya ijumaa ilionesha wazi kocha huyo hajapendezwa na kitendo cha Rashford kujiondoa kwenye timu ya taifa ya Uingereza kuelekea michuano ya kufuzu mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro.SouthgateImekua kawaida kwa Marcus Rashford kujiondoa kwenye timu ya taifa ya Uingereza marta kwa mara pale ambapo anaitwa hasa kwenye michezo ya kufuzu au kirafiki na kusema amepatwa na majeraha, Kutokana na tabia hii imekua haimfurahishi kocha wa timu hiyo.

Baada ya mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Italia kocha Southgate alisema hamna pengo lolote pale ambapo Marcus Rashford anakua hayupo kwenye timu hiyo, Kauli hii wengi wameitafsiri kama kocha huyo hapendezwi na tabia ya mchezaji huyo kutoka Manchester United.SouthgateKauli ya kocha Southgate pia imekutana na mapingamizi kutoka kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United mitandaoni ambao wanadai kocha huyo amekua hampi nafasi mchezaji huyo kwenye kikosi chake, Huku pia wakieleza kua mchezaji huyo ameshakwenda kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza mara kadhaa akiwa na majeraha hivo kocha huyo asimuandame mchezaji huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.