Wachezaji wa klabu ya PSG Leandro Parades na Julian Draxler waliopo kwa mkopo katika vilabu vya Juventus, na Benfica wanatarajiwa kurejea ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Parades alikwenda kwa mkopo klabu ya Juventus kwa msimu mzima ambapo amekua akionesha ubora mkubwa ndani ya miamba hiyo ya Serie A, Lakini atarejea ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu kuangalia mustakabali wake zaidi.
Mchezaji mwingine wa PSG aliepo klabu ya Benfica ya Ureno Julian Draxler raia a kimataifa wa Ujerumani, Lakini mchezaji huyo amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara hivo ni wazi klabu ya Benfica haitataka kumbakiza mchezaji huyo kutokana na tatizo la majeraha yake.
Leandro Parades licha ya kuwasha moto ndani ya klabu ya Juventus lakini inaelezwa kua miamba hiyo ya Italia haina mpango wa kumnunua jumla mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, Hivo kiungo huyo inabidi arudi jijini Paris majira ya kiangazi ili kuangalia hatma yake.
Leandro Parades na Julian Draxler wanatarajiwa kufanya mazungumzo na klabu yao ya PSG katika majira ya kiangazi, Ili kuangalia kama klabu hiyo ina mpango wa kuendelea nao na kama watahitajika kutimka klabuni hapo vilevile mazungumzo ndio yatatoa maamuzi ya mwisho ya wachezaji hao.

