Klabu ya Juventus iliyopo Italy wamefikia makubaliano na klabu ya Psg kumsajili Muargentina  Leandro Parades ambaye anacheza katika nafasi ya kiungo katika timu ya Paris Saint German ambao ndio mabingwa watetezi wa League 1.

Parades(28) Kwenda Juventus

Juventus watamsajili Parades kwa mkopo na na kifungu cha ununuzi cha takribani euro milioni 20 kwa Psg. Juventus walishabaliana makubaliano binafsi na mchezaji kwenye wiki ya kwanza ya mwezi August mwaka huu, kwani mchezaji mwenyewe alionesha nia ya kuitaka timu hiyo ya Juventus.

Vipimo vya afya vitafanywa siku ya Jumatano huko Paris, ndipo aanze safari ya kuelekea huko Italy kwaajili ya kusaini kandarasi klabuni hapo. Mchezaji huyo amekuwa akipata nafasi finyu sana katika kikosi cha Psg kutokana na kuwepo wachezaji wengi ndani ya klabu hiyo, na hata akipata nafasi hutokea benchi na sio kuanza moja kwa moja.

Parades(28) Kwenda Juventus

Parades anaenda kujiunga na Juventus ambao mpaka sasa wapo nafasi ya 8 Seria A wakiwa wamecheza mechi tatu ushindi mara moja na sare mbili huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa. Na leo hii watakuwa nyumbani kuwakaribisha Spezia.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa