Klabu ya Everton wamesema kuwa mchezaji wao Antony Gordon hatoondoka msimu huu wa joto licha ya kuwa Chelsea kumtaka kwa ushawishi mkubwa. Chombo cha habari cha michezo Uingereza kimeambiwa kuwa hakuna mahali yoyote klabu hiyo imezingatia kuondoka kwa mchezaji huyo.

Gordon Hatoondoka Everton 2023

Mchezaji huyo ambaye anacheza katika eneo la ushambuliaji amekuwa akihusishwa kujiunga na Chelsea ambao wamekuwa na uhitaji mkubwa wa wachezaji eneo hilo baada ya kuondekewa na wachezaji wake lakini kwasasa inaonekana kuna ugumu wa kumpata Gordon ambaye ana umri wa miaka 21.

Antony Gordon amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika klabu yake ya Everton anayocheza ndio maana amekuwa na mvuto kwa klabu ya Chelsea kumtaka licha ya klabu hiyo kutokuwa na matokeo mazuri wanayoyapata toka ligi kuu ya England iliporejea.

Gordon Hatoondoka Everton 2023

Klabu hiyo ipo chini ya kocha Frank Lampard ambaye alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Chelsea na kupata mafanikio makubwa klabuni hapo. Mpaka sasa Everton hawajashinda hata mechi moja katika michezo mitano waliyocheza, wamepoteza mechi mbili na sare tatu. Ambapo sare ya tatu  wameipata jana dhidi ya Leeds United ugenini, huku goli lao likifungwa na Antony Gordon.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa