London: Kocha mkuu wa Klabu ya Chelsea Thomas Tuchel ametoa neno hapo jana baada ya kupoteza mchezo wao wa jana ambao walikuwa wakikipiga dhidi ya vijana wa Saint Marrys Park( Southhampton) ambao walipoteza 2-1.

Tuchel: Sisi Sio Wagumu Kama Timu.

“Sisi Sio Wagumu Kama Timu”.

Tuchel amewawakia wachezaji wake  kutokana na mwenendo wa timu yake unavyokuwa toka ligi aanze jinsi ambavyo inafungwa kiulaini, na jinsi ambavyo hawazuii vizuri  matokeo hayaridhishi hata timu ikishinda lakini bado ushindi wanaoupata haushawishi. The Blues imepoteza mechi ya pili mfululizo ya ugenini huku ya kwanza ni ile aliyopoteza dhidi ya Leeds United kwa mabao matatu kwa sifuri na mechi ya jana akipoteza dhidi ya Soton kwa mabao mawili kwa moja.

Tuchel: Sisi Sio Wagumu Kama Timu.

Chelsea wanapitia katika hali ngumu kutokana na majeraha kwa baadhi ya wachezaji, lakini pia uchezaji mbovu,  kutosajili wachezaji katika maeneo mbalimbali likiwepo eneo la ushambuliaji ambalo nafasi zinatengenezwa nyingi lakini hakuna wachezaji wazuri mbele wakumalizia na hata waliopo wanazikosa sana nafasi hizo zinazotengenezwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa