Kroos na Alaba Kuandika Rekodi Real Madrid Ikishinda Copa de le Rey

Wachezaji wa klabu ya Real Madrid kiungo Toni Kroos na beki David Alaba wataandika rekodi ya kuingia kwenye orodha ya wachezaji walioshinda kila taji ngazi ya klabu wakiwa na vilabu viwili tofauti endapo Real Madrid itashinda taji la Copa de le Rey kesho.

Toni Kroos alifanikiwa kushinda kila taji akiwa ndani ya klabu ya Fc Bayern Munich akishinda taji la Bundesliga, DFB Pokal, taji la ligi ya mabingwa ulaya, pamoja na taji la klabu bingwa ya dunia vilevile ndani ya Real Madrid hajawafanikiwa kushinda taji la Copa de le Rey tu.KroosBeki David Alaba ambaye ameitumikia klabu ya Bayern Munich kwa kipindi cha muda mrefu na kushinda kila taji ambalo amelishindania ndani ya klabu hiyo, Akiwa na msimu wa pili tu ndani ya klabu ya Real Madrid amebakisha taji moja tu awe amefanikiwa kushinda kila taji ndani ya klabu hiyo.

Toni Kroos na David Alaba wote wamefanikiwa kucheza pamoja ndani ya klabu ya Bayern Munich na wakiandika rekodi pamoja ndani ya timu hiyo kwa kushinda kila taji ndani ya vigogo hao wa soka nchini Ujerumani, Lakini wamekutana tena ndani ya Real Madrid na wanaweza kuweka rekodi kwa pamoja tena.KroosKiungo Toni Kroos amejiunga na klabu ya Real Madrid mwaka 2014 mpaka sasa ameshafanikiwa kushinda taji la La liga, Spanish Super Cup, na taji la ligi ya mabingwa ulaya kama ambavyo David Alaba amefanikiwa kushinda ndani ya misimu yake miwili ya kwanza klabuni hapo na wakiwa wmaebakiza taji moja ambalo bi Copa de le Rey ambapo fainali yake itapigwa kesho dhidi ya Osasuna.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.