Haaland Mchezaji Bora wa Mwezi Aprili Epl

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa nne kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kua na kiwango bora zaidi ndani ya mwezi huo.

Earling Haaland amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya mwezi wa nne baada ya kuhakikisha klabu yake ya Manchester City kuvuna alama zote kumi na mbili kwenye michezo minne ambayo amecheza ndani ya mwezi huo, Huku vilevile akihusika na mabao nane katika michezo hiyo minne.HaalandMshambuliaji huyo amefanikiwa kufunga mabao sita katika michezo minne ambayo amecheza ndani ya mwezi wa nne, pia amefanikiwa kupiga pasi mbili za mabao kwa wenzake hivo kumfanya kua na mchango wa mabao nane katika michezo minne aliyocheza hivo kumfanya kua na takwimu bora kuliko wengine alioshindana nao.

Haaland anafanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwenye ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya pili baada ya kushinda kwenye mwezi wa kwanza wa ligi ilipokua inaanza mwezi wa nane, Hivo imemchukua takribani miezi saba tena mpaka kuchukua tuzo hiyo.HaalandMshambuliaji Haaland amekua na msimu bora sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza ikiwa mpaka sasa ameshafanikwa kufunga mabao 35 ikiwa ni rekodi ya kipekee ambapo haikuwahi kutokea mshambuliaji kufunga mabao hayo kwenye msimu mmoja kwenye ligi hiyo, Huku akiwa na nafasi ya kuongeza mabao zaidi kwani mpaka sasa imebaki michezo minne mpaka msimu utamatike.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.