KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ameweka wazi kuwa hana tatizo na Yanga bali kuna masuala ambayo amekuwa akifanyiwa na viongozi hayapendi. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.
Nyota huyo kwa sasa yupo kwenye mvutano na mabosi wa timu hiyo kuhusu suala la mkataba wake ambapo yeye anahitaji kuondoka huku Yanga wakiweka wazi kuwa mkataba wake bado unaishi mpaka 2024.
Feisal kwa sasa yupo nje ya uwanja akiwa Zanzibar na ameomba mchango kwa ajili ya kupata fedha ili akafungue kesi mahakama ya michezo ya CAS. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Aidha kwenye mahojiano na moja ya Redio kubwa Tanzania, ameweka wazi kuwa hakuna timu ambayo inafanya mazungumzo naye kwa sasa zaidi anachohitaji ni kuwa huru. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
“Mimi nimeondoka Yanga kwa sababu ya manyanyaso, mashabiki wa Yanga mimi nawapenda, ila kuna kitu hawakijui ambacho kimenitoa Yanga, kuna aina ya manyanyaso ambayo hayavumuiliki.
“Kuna wakati niliambiwa nauza mechi na baadhi ya viongozi wa Yanga. Siwezi kurudi Yanga kwa sasa kwa kuwa ninahitaji kucheza na kufanya kazi nikiwa huru.
“Nilikaa na viongozi zaidi ya mara mbili kuomba kuvunja mkataba wangu na kwa kuwa kuna kipengele ambacho kinanipa ruhusa ya kuvunja mkataba nilirudisha fedha walizonipa kwa mafungu mara moja,” amesema Feisal Salum.
Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.

