Kiungo wa mpira Feisal Salum Feitoto ameelezea safari yake ya soka ilipoanzia hadi kujiunga na klabu ya Yanga ambayo kwa sasa hawana maelewani mazuri kwa sababu za kimkataba. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.
Feitoto alifanyiwa mahojiano na Clouds FM kuhusiana na maisha yake ya soka, na hapa anaelezea sakata lake la usajili kutoka JKU, ambapo vilabu vya Tanzania bara kama Azam FC, Simba SC na Yanga vilikiwa vinamtaka mwaka 2018 akiwa na umri wa miaka 18 hiyo ni baada ya kuonesha kiwango kizuri kwenye mashindano ya kombe la mapinduzi. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
“Simba walinifata kunisajili kwa dau la mil25 nikakataa mie nilikuwa nataka mil 60 TZS”.
“Mohammed Hussein Mmachinga aliniona wakati naongea na viongozi wa Simba, akawapigia simu Yanga na kuwaambia huyu mtoto mtamkosa Simba washaanza kumfatilia” Feitoto.
“Nilipigiwa simu na viongozi wa JKU wakanambia niende Kituo cha Polisi cha Chang’ombe, nilivyoenda nikakutana na viongozi wetu na wa Yanga, wakaniuliza nasikia ushasaini Singida Utd, nikawajibu Ndiyo”.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
“Singida nilisaini mkataba wa awali kwa Tsh mil 18, lakini waliniahidi kunipa mil 25, viongozi wa Yanga walinijibu hilo tuachie sisi lakini sasa cha ajabu Yanga wakanipa Tsh 10m” Feitoto alieleza kupitia kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM.
Sakata la Feitoto na klabu ya Yanga bado una kizungumkuti licha ya TFF, kumtaka mchezaji huyo kurudi kwenye timu yake kwakuwa bado mkataba wake ni halali. Lakini Feitoto hakuridhishwa na maamuzi hayo na sasa anajiandaa kwenda CAS kutafuta suluhu ya jambo hili. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.