Kiungo wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Croatia Matteo Kovacic inaelezwa yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Manchester City kwajili ya kutimkia klabuni hapo kwenye dirisha hili kubwa.
Kiungo Kovacic pamoja na kambi yake wako kwenye mazungumzo na klabu ya Manchester City kwajili ya kiungo huyo kuachana na Chelsea na kujiunga na mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza, Mpaka sasa kama kila kitu kitaenda sawa basi mchezaji huyo atajiunga na mabingwa hao wa Uingereza.
Klabu ya Chelsea chini ya kocha mpya Mauricio Pochettino wanahitahitaji kufanya mapinduzi kwenye timu hiyo na eneo mojawapo basi ni eneo la kiungo, Klabu hio inataka kumuachia kiungo huyo pamoja na wachezaji wengine kwenye eneo hilo kwajili ya kutengeneza timu nyingine ya tofauti kabisa.
Kiungo Kovacic ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2018 amefanikiwa kukaa klabuni hapo kwa takribani misimu mitano sasa, Lakini pia akifanikiwa kutwaa mataji kadhaa kama taji la ligi ya mabingwa ulaya, Uefa Super Cup, Klabu bingwa ya dunia hivo ni mchezaji ambaye alikua muhimu na alefanikiwa ndani ya timu hiyo.
Matteo Kovacic inaelezwa ameshafikia makubaliano ya maslahi binafsi na klabu ya Manchester City mpaka sasa, Huku Chelsea nao wakiwa tayari kumuuza kiungo hivo kinachosubiriwa ni klabu ya Man City kupeleka dau mezani kama litawaridhisha Chelsea basi mchezaji huyo atatimkia kwenye viunga vya Etihad.

