Mchezaji wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs ambaye kwasasa anakipiga klabu ya Everton Delle Alli amefunguka nini ambacho kimemfanya kupotea na kushuka uwezo kwa kiasi kikubwa.
Delle Alli wakati anafanya mazungumzo na gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville kwenye kipindi cha gwiji huyo na kusema kitu kilichomfanya kuonekana amepoteza ubora wake kwa kiasi kikubwa ni msongo wa mawazo.
Mchezaji huyo amekua chini ya kiwango kama misimu mitatu sasa ambapo hadi klabu ya Tottenham ililazimika kumuuza kwenda Everton, Lakini pia alishindwa kucheza kwa kiwango cha juu na kumtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Besiktas ya Uturuki.
Delle Alli ameeleza kua msongo wa mawazo ambao ulikua unamsumbua kwa muda mrefu ulimfanya kua mlevi wa kupindukia na ikawa sababu mojawapo ya yeye kushindwa kufanya vizuri uwanjani kwa kipindi kirefu sasa.
Mchezaji huyo ambaye amewahi kua mchezaji bora kijana kwenye ligi kuu ya Uingereza mara mbili na kufanya vizuri sana kwa misimu kadhaa Delle Alli ameweka wazi kwasasa anaendelea vizuri kwakua ametoka kupata matatibabu ya afya ya akili ambayo alikua anaendelea nayo kwa wiki kadhaa nyuma.

