KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa sababu kubwa ya kuwapeleka wachezaji wake kufanya mazoezi mchangani ni kwa ajili ya kuwaongezea utimamu wa mwili kuelekea katika michuano ya kimataifa.
Yanga juzi Jumatatu walifanya mazoezi yao katika fukwe za Coco yaliyosimamiwa na kocha huyo pamoja na benchi lake la ufundi.
Akizungumza kuhusiana na maamuzi ya kuwapeleka wachezaji wake mchangani, kocha Gamondi alisema: “Malengo makubwa ya timu kuileta kufanya mazoezi katika fukwe hii ni kwa ajili ya kuwaongezea utimamu wa miili wachezaji.
“Kama ambavyo tunafahamu timu inaenda kushiriki michuano ya kimataifa hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunapata utimamu mzuri wa miili yetu.
“Wachezaji wanatakiwa kuwa fiti na wanatakiwa kuupata uharaka zaidi, ndiyo maana tumewaleta huku. Tunaamini kuwa hili litawasaidia kwa kuwa wametoka kupumzika kwa siku mbili,” alisema Kocha Gamondi.

