Pepe Kutimkia Uturuki

Winga wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutimka Arsenal na kuelekea nchini Uturuki katika klabu ya Trabzonspor baada ya kukataa ofa za Saudia.

Nicolas Pepe mpaka sasa inafahamika kua hayupo kwenye mipango ya klabu ya Arsenal, Hivo klabu hiyo imeamua kumuachia na winga huyo yuko mbioni kuondoka klabuni hapo na kuelekea nchini Uturuki.pepeArsenal wanaelezwa kua wapo kwenye hatua za mwisho kumalizana na winga huyo ambaye walimtoa kwa mkopo msimu uliomalizika katika klabu ya Nice kwakua mchezaji huyo hayupo kwenye mipango ya kocha wa klabu hiyo.

Winga huyo alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2019 kwa ada kubwa ya uhamisho lakini hakufanikiwa kuonesha makali ndani ya timu hiyo mpaka kufikia kutolewa kwa mkopo msimu uliomalizika na klabu hiyo kuamua kumuachia kwasasa.pepeVilabu kadhaa kutoka nchini Saudia vinaelezwa vilionesha kumuhitaji mchezaji huyo lakini Pepe ameonesha kua hakuvutiwa kujiunga na vilabu hivo huku yeye akitoa kipaumbele kwa klabu ya Trabzonspor ya nchini Uturuki.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.