Azam FC Ugenini Dhidi ya Coastal Union

Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa kuvutia utakuwa ni kati ya Wanamangushi, Coastal Union dhidi ya Azam FC mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1:00 usiku.

 

Azam FC Ugenini Dhidi ya Coastal Union

Mchezo huo utapigwa katika dimba la Mkwakwani Tanga, ambapo Azam FC watakuwa wakihitaji pointi 3 muhimu hii leo baada ya kutoa suluhu kwenye mchezo wake wa ligi uliopita.

Wakati kwa upande wa Coastal Union naye anazitolea macho hizo hizo pointi tatu baada ya kutoa sare mchezo wake uliopita huku akiwa hajashinda mechi yoyote kwenye ligi mpaka sasa.

Vijana wa Dabo wanashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi kumi na michezo minne hivyo leo hii huu utakuwa mchezo wao wa 5 ambao endapo watashinda watakaa kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Azam FC Ugenini Dhidi ya Coastal Union

Wakati kwa vijana kutoka Tanga wao wapo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi wakitofautiana pointi moja pekee na anayeshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi.

Je leo hii Coastal anaweza kupata ushindi wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Matajiri wa Chamazi?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.