UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa bado wachezaji wao wawili hawajarejea kwenye uimara hivyo watakosekana kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union ambao unatarajiwa kupigwa kesho Ijumaa kwenye Dimba la Mkwakwani Tanga.
Mchezo uliopita wa Azam walipata suluhu ugenini dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.Kocha wa Azam FC, Yusuph Dabo ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wachezaji wao muhimu bado hawajatengamaa lakini hawana hofu wataendelea kupambana.
“Yannick Bangala na Price Dube hawa ni wachezaji wetu muhimu lakini bado hawajawa imara kutokana na kusumbuliwa na majeraha lakini waliopo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi ya kesho (leo).“Kikubwa mashabiki wasiwe na hofu wazidi kuwa pamoja nasi, tushikamane kwa pamoja tunaamini tutafanya vizuri mechi hiyo.”