ROBERTINHO ANA JAMBO LAKE SIMBA

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ana jambo lake ndani ya timu hiyo kwani imefichuka ameagiza benchi lao la ufundi kutumia michezo yao ya Ligi Kuu Bara kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa robo fainali ya African Football League dhidi ya Al Ahly.

Simba wanatarajiwa kuvaana na Al Ahly katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya African Football League ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakiwa ndiyo wawakilishi pekee wea Tanzania katika mashindano hayo mapya.ROBERTINHOKuelekea mchezo huo Simba watakuwa na michezo miwili ya Ligi Kuu Bara ambapo mchezo wa kwanza dhidi ya Prisons kabla ya kuvaana na Singida Fountain Gate Jumapili ya kesho kutwa.

Robertinho alisema: “Ni wazi kama timu tuna ratiba ngumu katika siku chache zijazo ambapo tutacheza na Tanzania Prisons, na baada ya hapo tutacheza na Singida Fountain Gate FC kabla ya kuanza majukumu ya mashindano ya African Football League.Robertinho“Hivyo ni wazi hatuna muda wa kupoteza tunatumia michezo ya ligi kama sehemu ya maandalizi yetu kuelekea michuano hiyo mipya mikubwa na muhimu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.