KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ametaja mambo matatu yaliyosababisha wapoteze mchezo wao wa juzi dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1.
Mchezo huo wa raundi ya nne ulipigwa Uwanja wa Highland Estate uliopo Mbarali mkoani Mbeya. Jana Jumatano.Gamondi alisema wamepoteza mchezo huo kwa kuwa wachezaji wake walishindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na huku akisisitiza kuwa wanastahili kupewa lawama.
Gamondi aliongeza mwamuzi wa mchezo hakutenda haki kwa madai kuna maamuzi yalikuwa yanawaumiza kwa kuwa aliwaangalia wapinzani wake zaidi katika mchezo huo kuliko suala la usawa wa mchezo.
“Hali hiyo imekatisha tamaa kwa wachezaji wangu, hatuwezi kuwatupia lawama waamuzi kwa sababu walifanya majukumu yao na wachezaji walishindwa kutumia nafasi walizozitengeneza na kuweza kufunga huku safu ya ulinzi ikifanya makosa.“Kumetokea changamoto nyingi kwenye mechi yetu, katika suala la kifundi zaidi ya mambo matatu kwetu yamepelekea kushindwa kupata matokeo ambayo yamepelekea tupoteze mchezo kwa makosa yetu,” alisema Gamondi.