CHAMA AWAPIGIA MAGOTI SIMBA, AAHIDI FURAHA

Staa wa Klabu ya Simba Clatos Chama amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo na wanachama kwa matokeo mabaya kwenye mashindano yote waliyocheza hivi karibuni na kutoa ahadi ya kuwa watawapa furaha kuanzia sasa.

 

CHAMA AWAPIGIA MAGOTI SIMBA, AAHIDI FURAHA

Chama amesema, wao kama wachezaji wanajua kuwa hawakupaswa kupata matokeo yale kutokana na ukubwa na ubora wa kikosi chao na kuwa wamekaa na kukubaliana kufanya vema kwenye mechi zijazo kwenye mashindano yote.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Chama alisema: “Poleni mashabiki kwa matokeo ambayo tumepata kwenye hizi mechi tatu zilizopita hatujacheza vizuri na matokeo yamekuwa mabaya na sisi wenyewe kama wachezaji tumeona kuwa hatujacheza vizuri na hatustahili kupata matokeo kama yale.”

CHAMA AWAPIGIA MAGOTI SIMBA, AAHIDI FURAHA

Nafikiri muda huu ni wakati wa kuwapa furaha mashabiki na wanachama na tunaomba sapoti yao kubwa kuanzia sasa. Wachezaji wote tumekubaliana kuwa hatutakiwi kufanya tena makosa kama yaliyojitokeza.

Hatuwezi kuonyoosheana vidole kwa mmoja mmoja au labda kuna ugomvi au wengine hawaelewani na wengine sio hivyo na sio kweli. Alisema Chama.

CAF Champions League iliyopita tulianza na mechi ya Horoya tukapoteza, tukaja nyumbani tukacheza na Raja tukapoteza mwisho wa siku tukapambana na tukafuzu kwenda hatua inayofuata.

CHAMA AWAPIGIA MAGOTI SIMBA, AAHIDI FURAHA

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

“Ombi kwa mashabiki waendelee kutusapoti na wasione kama kuna ugomvi wowote, tushikane mikono ili Simba SC irudi nyakati zake za furaha.”

Mbali na Chama, kiungo wa timu hiyo Kibu Denis naye alitoa ya moyoni kwa kusema kuwa akiri kwenye michezo yao mitatu hawajafanya vizuri jambo ambalo linawaathiri hadi wao wachezaji.

Na kitendo hicho kinawaumiza sana, wanajua hadi mashabiki zao wa Simba SC hawajapendezwa na hayo matokeo kwasababu sio kawaida.

CHAMA AWAPIGIA MAGOTI SIMBA, AAHIDI FURAHA

“Kwenye maisha hauwezi kuwa na nyakati nzuri siku zote lazima utapitia misukosuko na siku zote kitu kizuri kikipitia kwenye mambo magumu halafu kikafanikiwa kujitoa kwenye hayo magumu ndipo kitaonekana hiki kitu ni kizuri, niwaombe mashabiki zetu kwenye hiki kipindi kigumu lazima tuwe pamoja.” Alimaliza hivyo Kibu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.