KOCHA CADENA AFICHUA KUHUSU UGONJWA WA SIMBA

Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Daniel Cadena amesema kuwa anafahamu na kusikia malalamiko ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuhusu timu yao, lakini ukweli ni kwamba timu hiyo ilikuwa na shida kidogo ya utimamu wa mwili.

 

Cadena alisema kuwa, lakini kwa sasa timu yao haijafanya vizuri kwenye mechi zao za hivi karibuni, lakini watu waamini kuwa bado chama lao lina nafasi ya kufanya makubwa kwenye msimu huu wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Cadena ameisimamia timu hiyo kwenye mechi mbili baada ya kuondoka kwa kocha Robertinho, akisimamia timu dhidi ya Namungo kwenye Ligi Kuu na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kisha kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Asec Mimosas.

“Mashabiki inabidi waelewe kuwa bado tuna nafasi kubwa ya kubadili hali hii ya uchezaji kwakuwa tuna wachezaji wazuri zaidi, kipindi hiki tunapaswa kuwa pamoja ili kurudi vizuri mechi inayofuata, wakati mwingine mpira una matokeo usiyotarajia.”

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Shida yetu ilikuwa ni kwenye utimamu wa mwili kidogo kwa wachezaji, lakini kwa sasa unaona kuna kazi tunafanya ili kuweza kufika kwenye matarajio yetu na nafasi ya kufanya hivyo bado kubwa sana. Alisema kocha huyo.

Acha ujumbe