TRY AGAIN ATOA TAMKO ZITO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Muhene (Try Again) amefunguka kuwa kwa sasa wanakwenda kwenye ukurasa mpya na klabu hiyo baada ya kuandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

Jana, November 26, Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC pamoja na wachezaji wa Simba walifanya kikao cha takribani siku nzima. Kikao ambacho kilianza majira ya saa saba mchana na kumalizika saa sita usiku, kikao ambacho kilikuwa na lengo la kufahamu changamoto zilizopo pengine zinazosababisha kupitia kwenye matokeo mabaya kwa hivi sasa.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah Try Again pamoja na Mwekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu na kwa mujibu wa taarifa kikao hicho kimepata muafaka na mipango ya kuyafikia malengo yao waliyoyalenga msimu huu.

Kwenye Kikao hicho wachezaji wa Simba waliahidi kuipambania nembo ya Simba SC, pamoja na kuyafikia malengo ambayo ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kurejesha furaha kwa mashabiki wao.

Kikao hicho kimeamua kutengeneza ukurasa mpya baada ya magumu ambayo wamepitia Simba SC ndani ya michezo mitatu iliyopita. Ikiwemo kula chuma 5-0 mbele ya Yanga, sare ya 1-1 na Namungo na kisha sare ya 1-1 na Asec Mimosas kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya kikao hicho Try Again aliandika kwenye Instagram yake: “Ukurasa Mpya.”

Moja ya wajumbe wa bodi ya Simba ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema: “Kauli ya mwenyekiti wetu ina maana kubwa sana, sasa tunakwenda kufanya makubwa na timu yetu imefungua ukurasa mpya wa kuyafikia malengo yetu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.