Simba Yafungiwa Kusajili kisa Sakho

Klabu ya Simba imefungiwa kufanya usajili na shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) baada ya kushindwa kulipa kiasi cha pesa walichokua wanadaiwa na klabu ya Teungueth.

Klabu ya Simba inadaiwa haikumaliza pesa wakati wanamsajili aliyekua mchezaji wa klabu hiyo Ousmane Sakho mwaka 2021, Hivo kupelekea klabu ya Teungueth kupeleka madai yake FIFA.simbaWekundu hao wa msimbazi ni wazi hawataweza kufanya usajili wa iana yeyote mpaka pale watakapolipa kiasi cha pesa ambacho wanadaiwa na klabu ya Teungueth kutoka nchini senegal.

Wekundu wa msimbazi wanapaswa kufanya kila linalowezekana kulipa kiasi hicho cha pesa wanachodaiwa, Kwani dirisha dogo la usajili mwezi Januari linakaribia hivo hawataweza kusajili kama hawatalipa kiwango hicho cha pesa.simbaWakati FIFA wameifungia Simba kufanya usajili wa kimataifa TFF wao wameifungia klabu hiyo kufanya usajili wa ndani, Hivo klabu hiyo itakua kwenye wakati mgumu kama watashindwa kulipa kiasi hicho cha pesa ambacho wanadaiwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.