Mdamu Bado Ana Ndoto za Kucheza Mpira

NYOTA Gerald Mdamu aliyewahi kukipiga ndani ya Polisi Tanzania bado anapambania hali yake ili kurejea kwenye ubora wake mdogomdogo baada ya kuumia mguu walipopata ajali ya gari wakitokea mazoezini.

Julai 9 2021 ilikuwa ni ganzi ya maumivu kwenye ulimwengu wa mpira baada ya ajali hiyo kutokea na mchezaji aliyeumia zaidi kuliko wote alikuwa ni Mdamu.

Regan Senya mtu wa karibu wa Mdamu alisema kuwa mchezaji huyo anahitaji msaada kwa kuwa ana mahitaji pamoja na watoto ambao wanasoma huku akiwa bado na ndoto ya kurejea uwanjani.mdamuMdamu anaendelea vizuri na taarifa ya awali iliyokuwa inazungumzia kuhusu kupata msaada wa kutoa vyuma ilipokelewa vizuri. Vile vyuma ambavyo vilikuwa vinamsumbua vilitolewa bado vyuma vingine vimebaki.

“Tunahitaji pia kumpata mtaalamu wa mifupa ili afanikishe jambo lake la kurejea uwanjani. Bado ana ndoto za kucheza mpira kwa kuwa ni kitu ambacho anakipenda,”alisema.

Kwa watakaoguswa kumchangia Mdamu namba ni 0655670101 jina Juliana Malekela.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.