Klabu ya Bayer Leverkusen ambayo inakipiga kule ligi kuu ya Ujerumani, BUNDESLIGA imemtimua kazi ambaye alikuwa kocha wao Erik Ten Hag baada ya kukosa matokeo mazuri kwenye mechi mbili alizocheza hadi sasa.

Kocha huyo kwenye mechi mbili alizocheza, amefanikiwa kupata pointi 1 kati ya 6 huku mechi ya kwanza akipigika akiwa nyumbani na mechi ya pili akitoa sare licha ya mpinzani wake kuwa na kadi nyekundu.
Leverkusen kwenye mechi ya kwanza ambayo walipoteza dhidi ya Hoffenheim wao ndio walitangulia kupata bao kabla ya kufanyiwa comeback na kupoteza wakiwa nyumbani. Lakini mechi ya pili hali ilikuwa hivyo hivyo walianza vyema kwa kuongoza na baadae wakaishia kutoa sare.
Klabu hiyo ilimuajiri Ten Hag akiwa kama kocha huru baada ya kachana na klabu ya Manchester United ambayo waliona kuwa hataweza kuwafikisha kwenye nchi ya ahadi wao kama timu kubwa Uingereza na Duniani kote lakini pia ni klabu yenye mashabiki wengi.


