Waamuzi wasaidizi wawili wamefungiwa kufuatia makosa ya kutafsiri sheria za mpira wa miguu katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Young Africans SC uliochezwa Visiwani Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan Complex. Uamuzi huo umefikiwa baada ya tathmini ya matukio kadhaa yaliyoibua mjadala wakati wa mchezo huo mkubwa wa ligi.

Msaidizi namba moja wa mchezo huo, Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam, amefungiwa kwa kipindi cha miezi sita baada ya kubainika kufanya kosa katika dakika ya 70 ya mchezo. Katika tukio hilo, alikataa bao halali la Simba akidai kulikuwa na kuotea kabla ya mpira kufungwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, baada ya wataalamu wa sheria za mpira wa miguu kuchambua tukio hilo kwa kutumia video ya mchezo, ilibainika kuwa hakukuwa na kuotea katika tukio hilo. Matokeo yake, uamuzi wa mwamuzi huyo ulithibitishwa kuwa wa makosa na kusababisha adhabu hiyo kutolewa.
Wakati huohuo, msaidizi namba mbili wa mchezo huo, Hamdan Said kutoka Mtwara, naye amechukuliwa hatua za kinidhamu na kufungiwa kwa miezi mitatu. Adhabu hiyo imetokana na kushindwa kutafsiri ipasavyo sheria ya kuotea katika dakika ya 61 ya mchezo.

Katika tukio hilo, alionesha kuwa mshambuliaji wa Young Africans, Prince Dube, alikuwa ameotea wakati timu yake ikifanya shambulizi dhidi ya Simba. Uamuzi huo ulisababisha shambulizi la Yanga kusimamishwa licha ya kuwa lilikuwa linaendelea kwa hatari kuelekea langoni.
Baada ya uchunguzi wa video ya tukio hilo kufanywa na wataalamu wa sheria za mpira wa miguu, ilithibitika kuwa mshambuliaji huyo hakuwa ameotea wakati mpira unapigwa. Kutokana na makosa hayo mawili, waamuzi hao wameadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu inayohusu udhibiti na nidhamu ya waamuzi.

