Nyota wa Brazil, Neymar Jr, ameweka wazi masikitiko yake baada ya kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichotangazwa na kocha Carlo Ancelotti. Licha ya kurejea uwanjani na kucheza dakika 90 kamili akiwa na Santos FC, bado mshambuliaji huyo hajafanikiwa kumshawishi kocha kuwa yupo katika kiwango bora cha kimwili.

Neymar, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Brazil, alikuwa miongoni mwa majina makubwa yaliyokosekana kwenye kikosi hicho, jambo lililozua mjadala mkubwa. Hii ni licha ya kuonyesha dalili za kurejea kwenye kiwango chake baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi ya bao katika mechi mbili za hivi karibuni.
Kocha Ancelotti ameweka wazi msimamo wake kwamba majina makubwa hayatoshi kupata nafasi kikosini, akisisitiza umuhimu wa utimamu wa mwili. Amesema wazi kuwa anahitaji wachezaji waliopo asilimia 100, akimaanisha kuwa Neymar bado ana kazi kubwa ya kufanya ili kurejea katika kiwango kinachohitajika kimataifa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza katika tukio la Kings League Brazil, Neymar hakuficha hisia zake, akieleza kuwa amesikitishwa na uamuzi huo lakini ataendelea kupambana. Amesisitiza kuwa ataendelea kujituma katika mazoezi na mechi ili kuhakikisha anarudi kwenye kikosi hicho kabla ya uteuzi wa mwisho kuelekea michuano ya FIFA World Cup 2026.

Kwa sasa, muda unazidi kuyoyoma kwa Neymar kuthibitisha ubora wake kabla ya kikosi cha mwisho kutangazwa Mei 19. Wakati huo huo, Brazil itacheza mechi za kirafiki dhidi ya Ufaransa na Croatia bila uwepo wake, huku yeye akibaki na jukumu la kuonyesha uwezo wake akiwa klabuni ili kurejesha imani ya benchi la ufundi.

