Neymar Aachwa Kikosi cha Brazil, Ancelotti Aeleza Sababu

Mshambuliaji nyota Neymar ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichotangazwa na kocha Carlo Ancelotti kwa ajili ya michezo ya kirafiki ya mwezi Machi, huku maandalizi ya Kombe la Dunia 2026 yakiendelea kushika kasi.

Neymar Aachwa Kikosi cha Brazil, Ancelotti Aeleza SababuBrazil wanatarajiwa kucheza dhidi ya  timu ya taifa ya France Machi 26 mjini Boston na baadaye kukutana na  timu ya taifa ya Croatia Machi 31 huko Orlando, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano hiyo itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kutokuwepo kwa Neymar kunahusishwa na hali yake ya kiafya, baada ya mchezaji huyo wa miaka 34 kukosa mchezo wa hivi karibuni wa Santos FC kutokana na uchovu wa misuli, hali iliyomzuia kocha Ancelotti kumpima kwa karibu kabla ya kutangaza kikosi.

Neymar Aachwa Kikosi cha Brazil, Ancelotti Aeleza SababuAkizungumzia uamuzi huo, Ancelotti alisema kuwa bado anamuhitaji Neymar lakini si katika hali yake ya sasa, akisisitiza umuhimu wa mchezaji huyo kuwa fiti kabisa kabla ya kurejea kikosini.

“Neymar anaweza kucheza Kombe la Dunia kama atakuwa katika kiwango cha asilimia 100. Sikumuita kwa sababu bado hajawa fiti kikamilifu. Anapaswa kuwa anafanya mazoezi na kucheza mara kwa mara,” alisema Ancelotti.

Neymar Aachwa Kikosi cha Brazil, Ancelotti Aeleza SababuPamoja na hilo, kocha huyo amemjumuisha kinda Endrick pamoja na kumpa nafasi ya kwanza Igor Thiago, huku majina mengine makubwa yakijumuisha Vinicius Junior, Raphinha na Gabriel Martinelli, wakilenga kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea michuano mikubwa ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.