Mshambuliaji wa PSG, Ousmane Dembele, ameitaka timu yake kucheza kwa kushambulia bila huruma dhidi ya Chelsea katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
PSG wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 5-2 walioupata katika mchezo wa kwanza jijini Paris, hali inayowapa nafasi kubwa ya kutinga robo fainali, huku Chelsea wakikabiliwa na kazi ngumu ya kupindua matokeo hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Dembele amesisitiza kuwa licha ya kuwa mbele kwa mabao matatu, hawapaswi kucheza kwa kujihami bali wanapaswa kuendelea na falsafa yao ya kushambulia ili kuhakikisha wanapata ushindi mwingine.
“Kama tulivyosema baada ya mchezo wa kwanza, mtazamo wetu ni kushinda. Hatuwezi kubaki tukijilinda tu, tunahitaji kushinda. Tunapaswa kubaki makini kwa sababu Chelsea ni timu bora yenye uzoefu Ulaya,” alisema Dembele.
Kwa upande wake, kocha wa PSG Luis Enrique alikiri kuwa mchezo huo unaweza kuwa na changamoto, akirejea uzoefu wa msimu uliopita walipokaribia kupoteza faida kubwa dhidi ya Aston Villa, akisisitiza umuhimu wa kudhibiti mchezo na kasi yake.
“Ni mfano mzuri wa jinsi mchezo wa soka unavyoweza kubadilika. Lengo letu ni kushinda na kufunga mabao, lakini tunajua kutakuwa na nyakati ngumu, hivyo tunapaswa kuwa makini muda wote,” alisema Enrique.
Aidha, kocha huyo alipuuza mjadala kuhusu ‘huddle’ ya Chelsea kabla ya mechi, akieleza kuwa jambo hilo halina tatizo iwapo kuna heshima kati ya timu hizo mbili, huku akisisitiza kuwa wanachojali zaidi ni matokeo ndani ya uwanja

