Mshambuliaji nyota wa FC Barcelona, Robert Lewandowski, anaripotiwa kuwa tayari kupunguza mshahara wake ili kuendelea kusalia klabuni hapo katika hatua za mwisho za maisha yake ya soka. Licha ya kuvutiwa na ofa nono kutoka ligi ya Marekani (MLS) pamoja na vilabu vya Saudi Arabia, nyota huyo wa Poland ameweka mbele ustawi wa familia yake ambayo tayari imezoea maisha ya Catalonia.

Lewandowski ameonyesha wazi nia ya kuongeza mkataba wake katika dimba la Spotify Camp Nou, hata kama italazimu kupokea malipo madogo kuliko anavyopata sasa. Klabu kama Chicago Fire FC zimekuwa zikimuwania, lakini mshambuliaji huyo anaonekana kutotaka kufanya mabadiliko makubwa kwa sasa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akiwa anakaribia kutimiza miaka 38 mwezi Agosti, Lewandowski anaonekana kuwa tayari kubadilika na hata kukubali nafasi ndogo zaidi kikosini ili kusaidia Barcelona kukabiliana na changamoto za kifedha zinazohusiana na sheria za matumizi (Financial Fair Play).
Mustakabali wake pia unahusishwa kwa karibu na wakala wake, Pini Zahavi, ambaye hivi karibuni alionekana Barcelona. Ingawa ziara yake ilihusiana zaidi na kumuunga mkono rafiki yake Joan Laporta katika uchaguzi wa urais, pia inatarajiwa kuwa atarejea mezani kwa mazungumzo ya mkataba mpya na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo.

Barcelona pia wanaangalia mustakabali wa kocha wao Hansi Flick, ambaye anaonekana kuwa nguzo muhimu ya mradi wa muda mrefu wa klabu. Hata hivyo, tofauti za kimtazamo kuhusu muda wa mikataba zinaweza kuwa changamoto, huku klabu ikihitaji uthabiti zaidi na kocha akipendelea mikataba ya muda mfupi.

