Chipukizi wa Chelsea FC, Estevao Willian, amevutia mashabiki baada ya kushiriki katika mahojiano ya burudani yaliyofanywa na GOAL, ambapo alitakiwa kuchagua kati ya nyota wakubwa wa England na Brazil. Katika mchezo huo wa “this or that,” kijana huyo alionyesha wazi upendeleo wake kwa wachezaji wa Brazil.

Katika nafasi ya golikipa, Estevao alimchagua Alisson Becker badala ya Jordan Pickford. Safu ya ulinzi pia ilifuata mkondo huo huo, akiwachagua Cafu dhidi ya Gary Neville, pamoja na Roberto Carlos dhidi ya Ashley Cole.
Hata hivyo, Estevao alijikuta katika wakati mgumu alipoulizwa kuchagua kati ya magwiji wawili wa Chelsea FC, John Terry na Carlos Alberto Torres, pamoja na Frank Lampard dhidi ya Kaka. Katika chaguo hizi, alicheka na kukwepa kutoa jibu, akionyesha heshima kwa pande zote mbili.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika upande wa kiungo na ushambuliaji, Estevao aliendelea kuonyesha msimamo wake kwa kumchagua Zico dhidi ya Steven Gerrard, na Casemiro dhidi ya Paul Scholes. Pia alimchagua Ronaldinho mbele ya David Beckham bila kusita.

Katika kilele cha uchaguzi huo, Estevao alimchagua Pele dhidi ya Wayne Rooney, na Ronaldo Nazario dhidi ya Harry Kane, akimaliza kwa kuipa Brazil ushindi kamili katika kila kipengele, ishara ya wazi ya mapenzi yake kwa soka la nyumbani kwao.

