Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Eric Chelle, ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachoshiriki mashindano ya kirafiki ya mataifa manne mwezi huu, huku nyota Victor Osimhen na kipa Stanley Nwabali wakikosekana kwenye orodha hiyo.
Nigeria, mabingwa mara tatu wa Afrika, ambao walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye AFCON 2025 iliyofanyika Morocco, wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo pamoja na timu za taifa za Iran, Jordan na Costa Rica.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Nigeria, mashindano hayo ni sehemu ya mpango mpana wa kiufundi wa kuimarisha timu ya taifa kuelekea mashindano yajayo. Kikosi hicho kimejumuisha majina makubwa kama Ademola Lookman, Maduka Okoye, Akor Adams, Frank Onyeka, Igoh Ogbu pamoja na wachezaji wa Fulham akiwemo Alex Iwobi na Calvin Bassey.
Kutokuwepo kwa Nwabali kunaelezwa kuchangiwa na hali yake ya kutokuwa na klabu kwa sasa baada ya kuvunja mkataba na timu ya Chippa United. Hali hiyo imewapa nafasi makipa Francis Uzoho na Adebayo Adeleye kujumuishwa kikosini.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo, Jordan wataanza kampeni yao dhidi ya Costa Rica Machi 27, huku Iran wakicheza na Nigeria siku hiyo hiyo. Siku nne baadaye, wenyeji watacheza dhidi ya Nigeria wakati Iran wakimalizia ratiba yao kwa kuvaana na Costa Rica.
Katika kikosi hicho, makipa walioteuliwa ni Maduka Okoye, Adebayo Adeleye na Francis Uzoho. Mabeki ni Calvin Bassey, Semi Ajayi, Bright Osayi-Samuel, Bruno Onyemaechi, Zaidu Sanusi, Igoh Ogbu na Emmanuel Fernandez.
Viungo ni Alex Iwobi, Frank Onyeka, Wilfred Ndidi, Raphael Onyedika na Fisayo Dele-Bashiru, huku washambuliaji wakiwa Ademola Lookman, Samuel Chukwueze, Moses Simon, Chidera Ejuke, Paul Onuachu, Akor Adams, Philip Otele na Collins Yira Sor.

