Nigeria, DR Congo Zapigwa Faini na FIFA Mechi za Kufuzu wa Kombe la Dunia

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limechukua hatua za kinidhamu dhidi ya Shirikisho la Soka la Nigeria na la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia matukio yaliyojitokeza katika mchezo wa mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 uliofanyika mwaka jana.

Nigeria, DR Congo Zapigwa Faini na FIFA Mechi za Kufuzu wa Kombe la DuniaMchezo huo wa fainali ulipigwa katika Uwanja wa Prince Moulay Hassan Stadium uliopo Rabat nchini Morocco, ambapo timu ya taifa ya DR Congo iliibuka na ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria na kufuzu hatua ya mchujo wa mabara.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa 

Katika mchezo huo, Meschack Elia aliifungia DR Congo bao la kusawazisha baada ya Nigeria kuanza kufunga kupitia Frank Onyeka. Bao hilo lilifanya mchezo kumalizika kwa sare kabla ya kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti, ambapo DR Congo ilifanikiwa kupata ushindi na nafasi ya kuendelea na hatua inayofuata ya mchujo.

Nigeria, DR Congo Zapigwa Faini na FIFA Mechi za Kufuzu wa Kombe la DuniaKwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya kinidhamu ya FIFA, mashirikisho yote mawili yalipatikana na hatia ya makosa tofauti yaliyotokea katika mchezo huo uliochezwa Novemba 16, 2025. Nigeria iliadhibiwa baada ya mashabiki wake kubainika kurusha vitu uwanjani, jambo linalokiuka vifungu vya 17 na 17.2.b vya Kanuni za Nidhamu za FIFA, na hivyo kutozwa faini ya faranga 1,000 za Uswisi.

Kwa upande wa DR Congo, mashabiki wake walibainika kutumia taa za laser au vifaa vingine vya kielektroniki wakati wa mchezo huo, kitendo kinachokiuka kifungu cha 17.2.d cha kanuni za kinidhamu za FIFA. Kutokana na tukio hilo, shirikisho la soka la nchi hiyo lilitozwa faini ya faranga 5,000 za Uswisi.

Nigeria, DR Congo Zapigwa Faini na FIFA Mechi za Kufuzu wa Kombe la DuniaWakati huohuo, Nigeria iliwasilisha malalamiko rasmi kwa FIFA Desemba 15, 2025 ikidai DR Congo ilitumia baadhi ya wachezaji wasio na sifa stahiki katika mchezo huo. Hati iliyowekwa wazi na mwanahabari Osasu Obayiuwana ilitaja majina ya wachezaji kadhaa waliocheza dhidi ya Nigeria, akiwemo Aaron Wan-Bissaka, Axel Tuanzebe na Cedric Bakambu.

Nigeria, DR Congo Zapigwa Faini na FIFA Mechi za Kufuzu wa Kombe la DuniaWakati DR Congo ikiendelea kujiandaa na mchujo wa mabara dhidi ya mshindi kati ya timu ya taifa ya New Caledonia au timu ya taifa ya  Jamaica, wachezaji Michel-Ange Balikwisha na Mario Stroeykens ambao walitajwa kwenye malalamiko hayo wameachwa katika kikosi kipya cha wachezaji 26 cha DR Congo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.