Kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, amesema ameumizwa sana na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Sunderland katika dabi ya Tyne-Wear, akisisitiza kuwa bado amejiweka kikamilifu kuinoa timu hiyo licha ya matokeo mabaya.
Matokeo hayo yamekamilisha wiki mbaya kwa Newcastle baada ya pia kutolewa kwenye UEFA Champions League kufuatia kichapo cha mabao 7-2 kutoka kwa Barcelona, huku wakishuka hadi nafasi ya 12 kwenye Premier League.
Ushindi huo umeifanya Sunderland kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya Newcastle katika ligi, wakiwa hawajapoteza kwa miaka 15 na kufikisha michezo 11 bila kufungwa katika dabi hiyo ya jadi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha Howe alikiri kuwa hana visingizio kutokana na kiwango kibovu cha timu yake, huku mashabiki wakionyesha kutoridhishwa kwa kupiga kelele za kukataa baada ya filimbi ya mwisho.
Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha Howe alisema “Ni maumivu makubwa sana, hasa kwa mashabiki wetu. Sina visingizio, hatukufanya vizuri na lazima tukubali lawama.”
Aliongeza kocha huyo “Nimejitoa kikamilifu kwa kazi hii, lakini nimevunjika moyo na kiwango changu na timu kwa wiki hii. Tunahitaji kujirekebisha haraka katika mechi zijazo.”

