Mbappe Afunguka Kuhusu Jeraha La Goti, Apinga Taarifa za Uongo

Nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé, amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa kuhusu hali ya jeraha lake la goti, akisisitiza kuwa hali yake inaendelea kuimarika.

Mbappe Afunguka Kuhusu Jeraha La Goti, Apinga Taarifa za UongoAkizungumza na vyombo vya habari, Mbappé alisema kuwa baadhi ya taarifa zilizoenea hazikuwa za kweli, huku akieleza kuwa hali hiyo ni sehemu ya maisha ya mwanasoka wa kiwango cha juu. Alieleza kuwa “Goti langu linaendelea vizuri na linaimarika kila siku. Kumekuwa na uvumi mwingi na taarifa zisizo sahihi, lakini hilo ni jambo la kawaida katika maisha ya mchezaji mkubwa.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikiri kuwa hapo awali alipata hofu kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata, lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, alipata utambuzi sahihi uliomuwezesha kuanza mchakato mzuri wa kupona.

Mbappe Afunguka Kuhusu Jeraha La Goti, Apinga Taarifa za UongoMbappé tayari amerejea uwanjani baada ya kukosa michezo minne ya La Liga, na sasa amepewa nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Brazil na Colombia.

Mbappe Afunguka Kuhusu Jeraha La Goti, Apinga Taarifa za UongoAkizungumzia malengo yake, Mbappé amesema yuko tayari kucheza mechi zote zilizosalia za Real Madrid kabla ya michuano ya Kombe la Dunia, akisisitiza kuwa anajisikia fiti na yupo tayari kwa changamoto zijazo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.