Bassey Ajiondoa Kikosi cha Nigeria Kutokana na Jeraha

Beki wa Fulham, Calvin Bassey, amelazimika kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kutokana na jeraha alilopata, akitarajiwa kukosa michezo ya kirafiki dhidi ya Iran na Jordan.

Bassey alikuwa anatarajiwa kuongoza safu ya ulinzi ya Super Eagles katika mashindano ya kirafiki ya mataifa manne yatakayofanyika Antalya, nchini Uturuki, lakini alijiondoa baada ya kupata maumivu ya mgongo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kupitia taarifa rasmi ya timu ya taifa ya Nigeria, ilithibitishwa kuwa mchezaji huyo hatakuwa sehemu ya kikosi hicho, ikisema “Calvin Bassey ameondolewa kwenye kikosi cha Nigeria kwa ajili ya michezo ijayo dhidi ya Iran na Jordan kutokana na jeraha la mgongo. Tunamtakia apone haraka.”

Kutokana na hali hiyo, Nigeria itawatumia mabeki wengine akiwemo Semi Ajayi, Bright Osayi-Samuel na Zaidu Sanusi pamoja na wengine, huku mchezaji mpya Emmanuel Fernandez akiitwa kwa mara ya kwanza kuziba pengo hilo.

Jeraha la Bassey linaweza kuwa pigo kwa Fulham katika harakati zao za kumaliza msimu wa 2025/26 katika nafasi za kushiriki michuano ya Ulaya, ambapo kwa sasa wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 44 baada ya michezo 31.

Bassey Ajiondoa Kikosi cha Nigeria Kutokana na JerahaWakati huo huo, nahodha wa timu hiyo Wilfred Ndidi amejiunga na wachezaji wenzake kambini kuchelewa kidogo, huku kikosi kikianza maandalizi ya mchezo wa kwanza dhidi ya Iran utakaochezwa Machi 27, kabla ya kukutana na Jordan siku nne baadaye.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.