Bodi ya Ligi Kuu ya NBC imetoa adhabu kali kwa mlinda mlango wa Yanga SC, Djigui Diarra, baada ya matukio ya dhidi ya mwamuzi na tabia isiyofaa katika mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Mtibwa Sugar fc.
Diarra amefungiwa mechi tatu (3) rasmi, adhabu ambayo inamlazimisha kutohudhuria michezo ya timu yake katika hatua muhimu za Ligi Kuu. Uamuzi huu umetolewa kufuatia matukio mawili yaliyochukuliwa kuwa makosa makubwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kosa la kwanza ni kumshambulia mwamuzi, jambo ambalo bodi ya ligi imeona kuwa lina hatari kubwa na linaweza kuathiri nidhamu ya mchezo kwa ujumla. Kosa hili limepewa uzito mkubwa kwa sababu unahusisha heshima ya maamuzi wa mchezo.
Aidha, Diarra pia ametozwa faini ya shilingi milioni mbili Tsh. 2,000,000/= kwa kosa la pili, ambalo ni kuonesha kidole cha kati wakati wa kuondoka katika eneo la uwanja, tabia inayopingana na maadili ya soka na kanuni za ligi.
Kwa jumla, adhabu hizo zinazojumuisha faini ya jumla ya shilingi milioni nne Tsh. 4,000,000/= ni ishara ya bodi ya ligi ya NBC kuimarisha nidhamu na kuhakikisha wachezaji wanaheshimu sheria na maadili ya mchezo.

