Diego Simeone Amsifu Griezmann Kabla ya Kuondoka Atletico

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amempongeza mshambuliaji Antoine Griezmann huku akijiandaa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu. Kauli hiyo imetolewa kabla ya mchezo wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya FC Barcelona.

Diego Simeone Amsifu Griezmann Kabla ya Kuondoka Atletico Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Atletico, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Orlando City SC inayoshiriki Major League Soccer baada ya msimu kumalizika.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo katika dimba la Camp Nou, Simeone alimuelezea Griezmann kama mchezaji mwenye nidhamu na mfano bora kwa vijana.

Diego Simeone Amsifu Griezmann Kabla ya Kuondoka Atletico Simeone pia alisisitiza mchango mkubwa wa Griezmann ndani na nje ya uwanja, huku akibainisha kuwa bado ana nafasi ya kuisaidia timu kufikia mafanikio zaidi, ikiwemo fainali ya Copa del Rey na hatua za juu za Champions League.
“Nataka kukushukuru kwa kazi yako, unyenyekevu wako na mwenendo wako mzuri kwa vijana,” alisema Diego Simeone. “Umetoa mengi kwa timu hii na kwangu wewe si mchezaji tu bali pia rafiki.”

Diego Simeone Amsifu Griezmann Kabla ya Kuondoka Atletico Kwa upande wake, Antoine Griezmann alisema “Ni heshima kubwa kucheza chini ya Simeone. Natumaini watu watakumbuka juhudi zangu na mchango wangu kwa timu.”

Hata hivyo, Griezmann alikataa kuzungumzia uhamisho wake kuelekea Marekani, akisisitiza kuwa kwa sasa anajikita kwenye mchezo dhidi ya Barcelona, timu aliyowahi kuitumikia kati ya mwaka 2019 hadi 2021.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.