Kocha wa Benfica, Jose Mourinho amesema hakuna mawasiliano yoyote kati yake na Real Madrid licha ya tetesi zinazoendelea kumhusisha na kurejea katika klabu hiyo ya Hispania msimu ujao.
Mourinho, ambaye aliwahi kuifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2010 hadi 2013, anatajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaoweza kuchukua nafasi ya kocha wa sasa Alvaro Arbeloa ambaye yuko hatarini kuondolewa baada ya timu hiyo kushindwa kutwaa taji kubwa kwa msimu wa pili mfululizo. “Hakuna mtu yeyote kutoka Real Madrid ambaye amewahi kuzungumza nami. Naweza kuthibitisha hilo,” alisema Mourinho.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa aliongeza kuwa amezoea kusikia taarifa za aina hiyo kutokana na muda mrefu aliokaa kwenye soka la kimataifa. “Nimekuwa kwenye mpira kwa miaka mingi sana, na nimezoea mambo kama haya… lakini hakuna chochote kutoka Real Madrid,” alisisitiza.
Wakati huo huo, Rais wa Real Madrid Florentino Perez alimchagua Arbeloa kuchukua nafasi ya Xabi Alonso mwezi Januari, lakini matokeo hayajawa ya kuridhisha huku timu hiyo ikiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi ya vinara Barcelona kwenye msimamo wa La Liga.
Real Madrid pia walitolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Bayern Munich, jambo lililoongeza presha kwa benchi la ufundi.
Mourinho, ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja uliobaki na Benfica, alisema anaendelea kujikita na majukumu yake ya sasa licha ya tetesi hizo. “Nina mwaka mmoja uliobaki kwenye mkataba wangu na Benfica, na hicho ndicho kilicho muhimu kwa sasa,” alihitimisha.

