Jumamosi hii inakuja na gemu kabambe sana katika ulimwengu wa soka. Hapa nimekuwekea gemu kali za wikiendi hii kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.
Tottenham v Arsenal

Spurs wanamkaribisha Arsenal kwenye dimba la Wembley, spurs wakiwa na hasira na kichapo walichokipokea kutoka kwa Chelsea hawatataka kulaza damu kabisa kwenye gemu hii, lakini matumaini ya kulinasa taji yamefifia mno.
Arsenal wao wanakomaa kuhakikisha wanajiwekea gemu kubwa dhidi ya Manchester United ambao wanapambana kumaliza kwenye 4 bora! Hata Hivyo Arsenal wataweza kuwakaribia Spurs kwa pointi nafasi kama wataweza kunyakua ushindi pale Wembley, watakuwa na tofauti ya pointi moja tu.
Bournemouth vs Manchester City
Bournemouth ametoka kupokea kichapo cha bao 5-1 kutoka kwa Arseanal, bila shaka hataki kurudia makosa anapokutana na Manchester City ambaye kwa sasa ana njaa ya kuwapindua Liverpool ambao wamekuwa wakipokezana kiti kwenye nafasi ya kwanza msimu huu.
Man City anahitaji kuitumia gemu hii kupata gemu 3 muhimu ili hata kama Liverpool akishinda gemu yake jumamosi hii basi waendelee kuwa na tofauti ndogo.
Manchester United vs Southampton
Manchester United wako kwenye fomu nzuri kama kawaida toka alipoingia kitengoni meneja wa msimu Ole Gunnar Solskjaer. Mpaka sasa Man U hawajapoteza gemu hata moja ya EPL wakiwa wamejiapiza kumaliza kwenye nne bora msimu huu. Ishu ya majeraha inatia wasiwasi zaidi kwa Man U wanapoelekea kupambana na Watakatifu hawa wana Southampton, lakini Ole Gunnar anaimani atasepa na pointi zote 3.
Tutupie macho moja ya Jumapili Everton vs Liverpool
Hii ni debi ya kati ya Everton na Liverpool. Hii ni tamu zaidi wakati Everton anahamu ya kumkwamisha Liverpool kuendelea kukimbiza za ligi hiyo kama akichukua pointi zote tatu. Liverpool wapo kwenye fomu nzuri zaidi wakiwa wametoka kuwalalua Watford bao 5-0. Liverpool wanataka kujihakikishia wanapunguza ushindani kwenye kiti walichokalia kwa kujiweka mbali kwa tofauti ya points dhidi ya Manchester City.
Unaonaje?
Hizi ndiyo gemu kali za jumamosi hii, je ni nani atateleza? ni Man City au Liverpool atakayempa ahueni mwenzake kwa kuruhusu kichapo? Vipi kuhusu Manchester United wataweza kutoboa kujiweka karibu zaidi na 4 bora msimu huu? Tottenham atakubali aibu nyumbani kwake?
Unaweza kufanya utabiri hapa moja kwa wa ligi hii! Bonyeza HAPA


Povel tz
Habar njem