Bale Bado ni Muhimu kwa Real -Solari.

Meneja wa Real Madrid, Santiago Solari anasema kuwa Bale bado ni sehemu muhimu ya klabu hiyo wakiwa wanajiandaa kuingia kwenye El Clasico nyingine.

Bale ameweza kuanza kwenye gemu 2 tu za LaLiga kwa mwaka huu 2019, alitumika kama sabu ya kipindi cha pili kwenye gemnu ambayo Real Madrid walipoteza kwa bao 3-0 ya fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona.

Kikosi cha Solari sasa kimepata nafasi nzuri ya kulipiza kichapo walichokipata kwa Barcelona wao wakiwa wenyeji wao kwa sasa japokuwa hasara ya kupoteza taji haitazibika. Meneja huyu anamtaja bale kuwa sehemu ya msingi ya klabu hii.

Bale Bado ni Muhimu kwa Real -Solari.
Bale anakosolewa kwa kiwango anachokionesha siku za hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa hatma ya Bale klabuni hapo imekuwa ikihojiwa na wadau wengi siku za hivi karibuni kwa sababu ya mwenendo wake wa soka ukionekana umedorora kidogo na pia akiandamwa na majeraha. Lakini meneja ana mtazamo tofauti dhidi ya staa huyu.

“ni muhimu, Bale amecheza mechi zote toka alipotoka kuuguza majeraha yake na amekuwa akifunga magoli” -Solari

Akizungumzia umuhimu wa staa huyu amewataja yeye pamoja na mastaa wengine Marcelo, Ansensio na Vinicius akiwataja wote kama wachezaji muhimu na anatarajia makubwa zaidi kutoka kwao.

Acha ujumbe