Mechi za LaLiga zitakuwa hazichezwi tena siku ya jumatatu! Hii ni taarifa kutoka kwa raisi wa shirikisho la soka la Uhispania bwana Luis Rubiales. Unaionaje hii mechi za LaLiga kutochezwa tena jumatatu?
Kwa mda sasa mashabiki wa soka wa Uhispania wanadaiwa kuwa walikuwa wanapinga kuchezwa kwa gemu siku ya Jumatatu. Gemu za LaLiga zinadaiwa kwa zilikuwa zinapangwa kuchezwa siku ya Jumatatu kwa sababu za kibiashara.
Mashabiki wa Alves walifanya mazishi ya utani baada ya ushindi wao kwenye gemu ya LaLiga wakipinga gemu za LaLiga kupangwa kuchezwa siku ya Jumatatu.

Hii sio mara ya kwanza mashabiki hawa kupinga uchezeshwaji wa mechi za LaLiga siku ya Jumatatu. Mashabiki hawa waliwahi kuandamana mwaka uliopita mwezi Disemba kupinga mechi kuchezwa siku za Jumatatu.
Kwa mujibu wa raisi wa Shirikisho hilo nchini Uhispania anasema gemu zote zitapangwa kuchezwa siku ya Jumamosi na Jumapili tu.
Mashabiki wanalalamikia kupuuzwa kwa mashabiki, wanasema licha ya biashara kuwa muhimu na mashabiki ni muhimu pia. Wanataka gemu zichezwe siku ya Jumamosi na Jumapili sio Jumatatu kwa lengo la kurusha kwenye talevisheni.
Raisi amesema hakutakuwa na mechi zozote Jumatatu tena, isipokuwa mechi zitapangwa Jumamosi na Jumapili kuanzia msimu ujao pia wanatazamia kuangalia nini kitawezekana kwa siku ya ijumaa baada ya majadiliano.

