Liverpool Mbioni Kumnasa Maxi Gomez

Liverpool wanaripotiwa kuwa katika matazamio ya kuamua kumnasa mshambuliaji wa Celta Vigo Maxi Gomez huku nyota huyu akidaiwa kupigiwa upatu na Luis Suarez.

Kwa mujibu wa The Sun, staa wa Barcelona mshambuliaji Suarez amekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na marafiki zake ambao wapo Real Madrid huku akipendekeza wamsajili staa huyo ambaye anafanya vyema kule Celta Vigo.

Gomez amechapa magoli 9 nkwenye gemu 24 alizoichezea Celta Vigo msimu huu ambao mpaka sasa wanashikilia nafasi ya 17 kwenye La Liga na wanajitahidi kujikwamua na rungu la kushuka daraja.

Staa huyu pia alicheka na nyavu mara 17 kwenye gemu 39 msimu uliopita na amecheza jumla ya gemu 9 kwa timu ya taifa ya Uruguay ambako alicheza pamoja na Luis Suarez.

Wakati staa huyu akihusishwa na klabu hii, West Ham pia walishajaribu kumsajili nyota huyu mwezi Januari lakini hawakuweza kulimaliza dili hilo.

Liverpool Mbioni Kumnasa Maxi Gomez
Maxi Gomez

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.