Bale Anawapa Hasara Real Madrid

Hali imekuwa sio Hali wakati matumaini ya Real Madrid kutwaa taji la LaLiga msimu huu yakitoweka. Baadhi ya wadau wamekuwa wakilaumu kuwa Bale hafanyi kazi ile ambayo anatarajiwa kufanya klabuni hapo huku akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara yanayomlazimizisha kuwepo nje ya dimba! Wakati haya yakiendelea thamani yta mchezaji huyu inadaiwa kushuka, hivyo kwa namna moja au nyingine nyota huyu anawapa hasara Real Madrid.

Nyota huyu alikuwa akitaniwa na mashabiki kama wanamzomea hivi wakati akitoka dimbani baada ya kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Barcelona kwenye gemu ya LaLiga pale Bernabeu.

Staa huyu aliingia Real Madrid kiangazi cha mwaka 2013 kwa paundi miliondi 90. Kwa msimu huu ameliona goli mara 13 kwa gemu 33 alizocheza kwenye michuano yote uwepo wa kinda anayefanya vizuri Vinicius Junior unahatarisha zaidi nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza ipo hatarini.

Kwa mujibu wa Transfermarket, ambayo inaeleza taarifa nyingi za wachezaji, mafanikio yao hasa hasa thamani zao inaonesha thamani ya nyota huyu kushuka hadi kufikia paundi milioni 63, dau ambalo ni pungufu ya karibia paundi milioni 30 lililolipwa na Real Madrid kumnasa staa huyu. Kama dau hilo ni sahihi kama thamani ya nyota huyu kwa sasa basi Real Madid wanakula hasara ya kiasi kilichopungua kwenye dau walilomnunulia wao.

Hata hivyo licha ya kuwa na kipindi kigumu klabuni Real, akionekana kama amepungua makali yake bado anahusishwa na klabu zenye pesa za Manchester United na Tottenham.

Akiwa Real Madrid unaweza kupima mafanikio yake pia kwa mataji aliyojikusanyia akiwa na wakali hao. Ameshinda taji LaLiga 1, Kombe la Hispania 1, na Ligi ya Mabingwa mara 4. Pia maechukua tuzo muhimu katika misimu mitatu iliyopita.

Hatma? hapa inategemea kama Real Madrid wataamua kumuuza nyota huyu kwa dau la hasara kiangazi kinachokuja au la! Lakini ripoti zinasisitiza Real wako tayari kumtoa kwa dau hilo.

2 Komentara

    hapa inategemea kama Real Madrid wataamua kumuuza nyota huyu kwa dau la hasara

    Jibu

    Duuh hatari sana

    Jibu

Acha ujumbe