Ni furaha United! Ushindi wa kihistoria wa Manchester United dhidi ya PSG umewatoa kimasomaso mashabiki wengi wa Manchester United ambao wanatembea kifua mbele huko kitaa! ‘Ebwanaa eenh kazi ya Ole Gunnar unaiona lakini’ -Ndiyo tambo za wanaoisapoti klabu hiyo huko mtaani! Waasisi wa klabu hiyo Eric Cantona na Alex Furgurson hawajaachwa nyuma wameungana na Ole Gunnar kusherekea mafanikmio haya.

Man United wamekuwa timu ya kwanza kutoboa kwenye hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa magoli kuanzia mawili au zaidi wakiwa kwao. Inakumbukwa walichapwa bao 2-0 wakiwa wenyeji wa PSG, lakini wameweza kujipindua na kushinda bao 3-1 ugenini, bao la ugenini limewapa nafasi ya kutoboa.
Eric Cantona, Furgurson na Ole Gunnar wote ni wataalam ambao tayari wamejijengea heshima kubwa kwenye maandiko ya historia ya labu hiyo. Bila shaka ushindi huu wa kihistoria una maana kubwa sana kwa wataalam hawa. Kwa pamoja wameamua kusherekea ushindi pale Parc des Princes!
Furaha inawakumbusha maajabu mengine!
Gemu hii imewakumbusha miaka 20 iliyopita, kipindi cha Sir Alex Ferguson, pale Ole Gunnar aliposhinda moja ya bao mashuhuri kabisa lililowapa ushindi dakika za majeruhi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Dhidi ya Bayern Munich


Povel
Ferguson ni kocha mwny heshima epl na united