Ili mpira ukubalike miongoni mwa wanamichezo na wapenda soka lazima kuwepo na watu wanaowashawishi kuwatazama pindi wakiwa uwanjani. Kutokana na hilo wanachangia wao kulipenda soka hilo. Pamoja na hilo kuna aina ya viungo ambao hufanya kazi ya pekee kunogesha soka. Timu yenye viungo walioshibana kwa kukaa muda mrefu wana uwezo wa kufanya makubwa hata wakiwa uwanjani.
Japo wapo ambao huwa katika mfumo mmoja unaoendana hata kama hawajakaa muda mrefu kikosini hapo. Baadhi ya klabu zenye kufikia kitu hicho huweza kuwa na mlolongo mzuri sana wa matokeo wenye magoli mengi ya kufunga kuliko kufungwa.
Jorginho, Kante & Kovacic
Ingeweza kuwa Barkley ndiyo anaweza kuchukua nafasi ya Mateo lakini kutokana na kikosi kilivyo na namna ambavyo viungo hao walivyokuwa na mzunguko mzuri katika eneo la kati pindi wanapocheza, uwepo wa Jorginho ndani ya kikosi hicho unachagizwa kwa kiwango kikubwa kikosi hicho kucheza mpira mwingi na wenye kuvutia.
Winks, Sissoko & Eriksen
Pochettino, bila shaka, anafutahia sana uwepo wa wachezaji hawa ndani ya kikosi cha wanakuwa na uwezo wa kumiliki sana mpira na kutengeneza mashambulizi mengi kutokana na kasi, uimara na akili za uwanjani walizonazo. Mipira mingi ya Eriksen inaonekana kwa macho kwa mchezaji kuweza kufunga tu na huonekana dhahiri.
Wijnaldum, Henderson & Milner
Pamoja na uimara walionao katika safu ya ulinzi lakini eneo jingine ambalo limekuwa tishio sana ni lile la kiungo ambacho kimekuwa mhimili mkubwa wa kukipa uhai kikosi chenye nia ya kupata ushindi angalau ndani ya msimu. Uwepo wao umetia chachu na hamasa iliyokuwepo ndani ya safu mbili yaani ulinzi na ushambuliaji.
Fernandinho, Silva & De Bruyne
Kwa hakika hii ni timu ambayo imekuwa na viungo wa kila aina yaani wale wanampa imani Pep. Wamekuwa wakicheza aina moja ya mchezo. Ni aina ya wachezaji ambao kila kocha anawatamani.
Casemiro, Modric & Kroos
Ni nguzo pekee iliyosalia katika kikosi kwa sasa kwa wachezaji wakongwe wenye majina makubwa. Wamekuwa moto wa kuotea mbali kikosini kwa kufanya kikosi kuonekana imara hata katika maeneo yenye mapungufu ya wazi. Kama safu ya ulinzi; uwepo wao umeweza kufuta kabisa kasoro hiyo hivi karibuni.


Furahav
Wako vizuri uingereza.