Huku ligi ya Uingereza ikiwa inaelekea mwishoni mwa mashindano yake, huku kila timu ikijaribu kupigana kujua itamaliza ikiwa nafasi ipi na nyingine zikijiandaa kushuka katika ligi yao, lakini vurugu la kufurukuta kusalia katika nafasi ya nne limekuwa kubwa sana huku klabu tatu zikiwa zinapigania kupata nafasi hiyo ambayo huashiria tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa.
Ufungaji wa magoli mara zote huashiria mafanikio kwa klabu lakini uwepo wa mlinda mlango bora anayepigana kuzuia timu yake isipoteza matokeo mazuri hupewa nafasi kubwa sana. Ili kutambua mchango wa aliye bora katika nafasi hiyo golikipa aliyefanya vizuri hupata nafasi ya kuchaguliwa katika kikosi cha Professional Footballers’ Association [PFA]. Kwa mwaka huu kuna ushindani wa walinda mlango sita wanaowania nafasi hiyo.
Neil Etheridge
Ndani ya msimu huu Cardiff ilianza vizuri kampeni zake za kutafuta nafasi za juu za ligi huku mlinda mlango wao mkuu akiwa ni Neil ambaye amefanya kazi kubwa sana hadi kuifikisha klabu yake hiyo katika nafasi hiyo. Ametajwa kuwania tuzo hiyo yenye heshima kubwa ndani ya taifa la Uingereza.
Ben Forster
Miongoni mwa vitu United wanaweza kujisifia ni kuwa na uzao mzuri wa magolikipa. Anakumbukwa kwa makubwa aliyoyafanya ndani ya kikosi hicho. Anafurahia msimu huu akiwa hajaruhusu goli katika mechi saba ndani ya ligi na kumfanya kuwa miongoni mwa waliotajwa kuwania.
Rui Patricio
Wolves walifanya usajili wa mlinda mlango huyo raia wa Ureno kutokana na uwezo aliouonesha akiwa kwenye timu ya taifa. Hadi sasa hajafungwa goli lolote ndani ya mechi sita miongoni mwa nyingine nyingi alizozicheza.
David de Gea
Hata kabla ya Ole alionesha ubora wake kwa kufuta makosa mengi yaliyofanywa na safu ya ulinzi. Hadi sasa anabaki kuwa bora kutokana na uimara wake ndani ya kikosi hicho huku akiwa amefanikiwa kutoruhusu goli katika mechi saba msimu huu.
Alisson Becker
Ameleta ubora fulani wa kipekee ndani ya kikosi cha Liverpool, huku akiwa na rekodi nzito ya uhamisho wake kutoka Roma. Ameanza mechi zake zote 28 za klabu huku akiwa hajaruhusu magoli katika mechi 16 ndani ya msimu huu.
Ederson
Ndani ya ligi hiyo asingekutana na upinzani wa Mbrazil mwenzake angewika sana katika taifa lao pia lakini ubora wa Alisson bado unamfanya angoje sana. Pia kwa nafasi yake hajafanya makubwa kama ya mwenzake. Kwa sasa Ederson amefanya kazi kubwa ya kuzuia magoli yasipite kwenye himaya yake katika mechi 14 za ligi hiyo msimu huu.

