Kinda wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi amepata shavu kwenye kikosi cha uingereza chini ya miaka 21 kwa mara ya kwanza wakati kikosi hicho kikiandaliwa kuvaana na Poland na Ujerumani kwenye Michuano ya Ulaya mwezi huu wa Machi.
Kinda huyu wa miaka 18 amecheza jumla ya gemu 16 za chelsea, lakini bado haanza rasmi kuchezea kikosi kikubwa cha klabu hii kwenye gemu za Ligi Kuu. Kwa gemu ambazo amecheza msimu huu ameweza kuonesha uwezo ubora wake na kuafanikiwa kuchapa magoli 4.
Uingereza wanajiandaa kuwakaribisha Poland pale Brstol City Machi 21 pia watavaana na Ujerumani pale Bournemouth Machi 26.
Kikosi Kizima cha Uingereza U21
Magolikipa: Freddie Woodman (Newcastle United), Angus Gunn (Southampton), Dean Henderson (Sheffield United, kwa mkopo toka Manchester United)
Walinzi: Jake Clarke-Salter (Vitesse, kwa mkopo toka Chelsea), Jay Dasilva (Bristol City, kwa mkopo toka Chelsea), Dael Fry (Middlesbrough), Lloyd Kelly (Bristol City), Jonjoe Kenny (Everton), Ezri Konsa (Brentford), Fikayo Tomori (Derby County, kwa mkopo toka Chelsea), Kyle Walker-Peters (Tottenham Hotspur), Aaron Wan-Bissaka (Crystal Palace)
Viungo: Harvey Barnes (Leicester City), Hamza Choudhury (Leicester City), Tom Davies (Everton), Kieran Dowell (Sheffield United, kwa mkopo toka Everton), Phil Foden (Manchester City), James Maddison (Leicester City), Ryan Sessegnon (Fulham)
Washambuliaji: Tammy Abraham (Aston Villa, kwa mkopo toka Chelsea), Dominic Calvert-Lewin (Everton), Demarai Gray (Leicester City), Callum Hudson-Odoi (Chelsea), Ademola Lookman (Everton), Reiss Nelson (Hoffenheim, kwa mkopo toka Arsenal), Dominic Solanke (AFC Bournemouth)

